• Android (toleo la Go)

    Inatumika kwenye vifaa vya msingi.

    Mfumo wa uendeshaji wenye kasi sana ulioundwa kwa ajili ya simu mahiri zenye RAM isiyozidi GB 2. Android (toleo la Go) hufanya kazi kwa kasi na huokoa data, hivyo inaweza kufanya mengi katika vifaa vingi.

  • Skrini inayoonyesha programu zikifunguliwa kwenye kifaa cha Android.

    Hufunguka haraka zaidi.

    Programu hufunguka kwa kasi ya asilimia 30 zaidi ukitumia Android (toleo la Go) kwenye simu mahiri za msingi.

  • Hufanya zaidi, kwa wakati mmoja.

    Ukiwa na hadi MB 270 za hifadhi ya ziada, unaweza kutumia programu na michezo zaidi kwa wakati mmoja.

  • Huweka nafasi ya ziada.

    Nafasi ya ziada ya hadi MB 900 inakupa fursa ya kuhifadhi picha, video na programu zaidi. Chagua kutoka zaidi ya programu milioni mbili kwenye Google Play.

Imebuniwa ili kuunganisha watu.

Tunaamini kuwa kila mtu anapaswa kufurahia utumiaji wa simu mahiri. Kuanzia hali ya ufikivu iliyoboreshwa hadi kuwa na uwezo mkubwa wa kumudu, Android (toleo la Go) huleta mabadiliko.

  • Kamera inayosoma maandishi kwa sauti.

    Lenzi katika Google Go husoma maandishi kwa sauti, na kuwasaidia watu wengi kuelewa ulimwengu unaowazunguka.

Kivinjari kinachozungumza lugha yako.

Chrome hutafsiri ujumbe wowote ulio kwenye skrini katika lugha yako. Soma kwa sauti, kwa kugusa kitufe tu.

Programu zinazoongeza fursa.

Kwenye Android (toleo la Go), programu maarufu za Google zinaundwa kikamilifu. Programu hutumia nafasi kidogo na huokoa data zaidi. Kila kipengee kina kasi, manufaa zaidi na ni rahisi kutumia.

Google Go

Kamera

Assistant Go

Dhibiti faili kwa urahisi.

Files by Google inamsaidia kila mtu kupata, kushiriki na kufuta maudhui yake. Pata vidokezo kuhusu maudhui ya kufuta kama vile programu zisizotumika. Unaweza pia kutuma faili kwa marafiki walio karibu bila kutumia data.

Pata usawa bora.

Zana za Nidhamu Dijitali zinakusaidia kudhibiti jinsi unavyotumia simu yako. Weka vikomo ukitumia Vipima Muda katika Programu na udhibiti arifa. Au punguza kukatizwa ukitumia kipengele cha Usinisumbue.

Zaidi kwenye Google Play.

Vipengele vya usalama vilivyojumuishwa vinavyotoa ulinzi wakati wote.

Android (toleo la Go) ina vipengele vya usalama vilivyojumuishwa vinavyomfanya kila mtu awe salama. Vimeidhinishwa na wataalamu kutoka Google.

Google Play Protect

Acha huduma hii ya ulinzi ijiendeshe yenyewe ili izuie programu hatarishi kufikia simu yako.

Tafuta Kifaa Changu

Tafuta, funga na uondoe (si lazima) data iliyo kwenye kifaa isipatikane kabisa iwapo kitapotea.

Vidhibiti zaidi vya faragha

Dhibiti data binafsi. Pata maelezo ili ufanye uamuzi bora wa chaguo za faragha.

Usalama bora

Weka data salama bila kuathiri utendaji ukitumia usimbaji fiche wa kina.

Buni programu za hadhira kubwa.

Fikia watu wengi kwa kuunda programu ukitumia Android. Jiunge na wasanidi programu wengi wanaounda programu zilizobuniwa ili kutumika kwenye simu mahiri za msingi.

Pata maelezo zaidi

Tutengeneze pamoja.

Zaidi ya asilimia 80 ya simu za msingi za Android zinatumia Android (toleo la Go). Katika nchi zaidi ya 180. Kwenye miundo zaidi ya 16,000. Pata zana unazohitaji ili uwasaidie watumiaji wafanye shughuli zaidi kwa kutumia Android.

ANZA